Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA
leo amezindua rasmiKampeni ya uhamasishaji wa Sensa ya watu na Makazi jijini
Dar es salaam zoeziambalo linatarajiwa kufanyika Agost 26 mwaka huu.
Amesema sensa haina mahusiano yoyote
na imani za dini isipo kuwa ni kutafuta idadi ya watu ili kupata taarifa
zitakazoweza kusaidia nchi katika kuleta na kupanga Maendeleo.
Amefafanua kuwa ni vema Umma ukahamasishwa
na kuelimishwa kwani sensa ni jambo jema.
Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais
Zanzibar Balozi SEIF ALI IDD amesema sensa inakabiliwa na changamoto kadhaa
ikiwemo uelewa mdogo kwa baadhi ya viongozi wadini na wananchi hali
inayopelekea kuwanyima wananchi haki yao ya msingi.
Balozi IDD amesema kutofanikiwa kwa
zoezi hilo wajue ni hasara kubwa kwa nchi hivyo kutokuwa na faida yoyote kwa
wale wanaohamasisha wananchi wasishiriki.
Naye Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Ndugu SAID MECKY SADIQ amesema kuna baadhi ya Mashekhe wanapita misikitini na
majumbani kuhamasisha watu wasijitokeze kushiriki zoezi huilo kwa madai kuwa
hakuna kipengele cha kuonesha wewe ni dini gani hivyo hoja hiyo ni dhaifu.
Zoezi la sensa linatarajiwa kutumia
zaidi ya Shilingi Bilioni 140 hadi kukamilika kwa zoezi la Sensa.



No comments:
Post a Comment