Katika
kuhakikisha uhalifu wa kimtandao unadhibitiwa na hata kumalizwa kabisa hapa
nchinik, wizara ya ya mambo ya ndani imepata msaada wa mafunzo maalum pamoja na
kukabidhiwa vifaa mbalimbali zikiwemo kompyuta, vyenye thamani ya dolari za kimarekani 75,000
kwa lengo la kupambana na uhalifu huo wa kimtandao ambao umeonekana kuanza
kusambaa kwa kasi nchini na duniani kwa ujumla.
Tafrija fupi
ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika ubalozi wa Marekani hapa nchini
tarehe 13/09/2012 na kuhudhuriwa na
maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi na wizara ya mambo ya ndani nchini wakiongozwa
na Kamishna Mwandamizi wa Polisi S.M KONDELA akimuwakilisha mkuu wa jeshi la
polisi nchini IGP Saidi Mwema.
Afisa
usalama wa kanda ya Afrika mashariki toka ubalozi wa Marekani Jeremy Yamin akimuwakilisha
balozi wa nchi yake hapa amesema lengo kubwa la kukabidhi vifaa hivyo ni
kuendeleza ushirikiano katika kukabiliana na uhalifu nchini.
Aidha amempongeza IGP Mwema kwa kufanikiwa kulibadilisha
jeshi la polisi kuwa la kisasa hatua ambayo inalifanya jeshi hilo kuwa na uwezo
wa kupambana na uhalifu kisayansi jambo ambalo linaweza kupunguza kama si kuumaliza kabisa uhalifu nchini.
Kwa upande
wake kamishina Kondela ameshukuru kwa msaada huo lakini pia jitihada kubwa
zinazo fanywa na Marekani katika kuimarisha hali ya usalama nchini ikiwa ni
pamoja na kuendesha semina kwa maafisa kadhaa kutoka wizara ya mambo ya ndani
ambazo zilikuwa na lengo la kutoa mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na uhalifu wa
kupitia mtandao wa kompyuta.
Vifaa vilivyo
tolewa ni kwa ajili ya kuboresha idara ya cyber crime na crime scene ambavyo
vinatarajiwa kuongeza ufanisi katika idara hizo nyeti inayo jihusisha na forensics.
Vifaa
vilivyo tolewa kama zawadi vina uwezo wa kubaini kwa urahisi wizi wa kwenye
mtandao na kukusanya vielelezo kutoka katika maeneo ya matukio ili kukuza
ufanisi katika kukabiliana na wahalifu nchini.
Vifaa
hivyo vilifungwa siku ya pili baada ya makabidhiano ya kufanyika
No comments:
Post a Comment