Mwalimu
Mboya akisindikizwa na walimu wenzake wakitoa msaada wa ndala dazani
moja, dawa za mswaki dazani mbili na miswaki dazani mbili. Kuanzia
kushoto ni Mwalimu Ana Kimatare, Mzee Hamisi Mwakimwagile (akiyepokea
msaada huo kwa niaba ya Tanzania 50 Plus Campaign), Mwalimu Florence
Mboya, Mwalimu Happy Lumbwe na Mwalimu Ng’walu Mipawa.
Tanzania
50 Plus Campaign ikishirikiana na waathirika wa saratani na marafiki
wa kampeni itatembelea hospitali ya wagonjwa wa saratani katika
hospitali ya Ocean Road Cancer Institute tarehe 24 Novemba 2012 saa 4
asubuhi. Ili kufanikisha zoezi hilo imeomba watu binafsi na makampuni
mbali mbali na jamii kwa ujumla kuchangia misaada ya sabuni za kufulia,
za kuogea, mafuta ya kujipaka (petroleum jelly), miswaki, dawa za
miswaki, ndala, maji ya kunywa, juice mbalimbali na mtunda.
Tanzania
50 Plus Campaign inamshukuru sana Mwalimu Florence Mboya kwa ukarimu
wake na moyo wa upendo na huruma kwa wale wenye mahtaji. Bado
tunaendelea kupokea misaada.
Ukiwa na msaada wako wasiliana nasi:
Simu 0754 402033
au barua pepe: chrptz@yahoo.com,
ekandusi@yahoocom
No comments:
Post a Comment