Bunge nchini Somalia
limeidhinisha baraza jipya la mawaziri kumi waliloteuliwa na waziri mkuu Abdi
Farah Shirdon. Wanawake wawili ni miongoni mwa walioteuliwa.
Serikali kwa mara ya kwanza ina waziri wa kwanza mwanamke
atakayeshikilia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje, Fauzia Yusuf Haji Adan na
ambaye anatoka Somaliland.
Kuidhinishwa kwa baraza hilo kumekuja licha ya ripoti kuwa
baadhi ya koo hazikuwakilishwa vyema kwenye baraza hilo liliotajwa wiki moja
iliyopita.
"Wabunge walipitisha baraza hilo kwa kura 219 , kati ya
wabunge 225, waliohuduhuria kikao'' alisema spika wa bunge Mohamed Osman
Jawari.
Wabunge watatu waliwakataa mawaziri hao huku wengine watatu
wakijizuia kupiga kura.''
Rais mpya pamoja na wabunge wapya walichaguliwa hivi
karibuni nchini Somalia , nchi iliyokuwa haina serikali thabiti kwa zaidi ya
miaka 20.
Serikali mpya inakabiliwa na changamoto nyingi wakati
ikijaribu kuleta utulivu na utahbiti katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na vita
vya muda mrefu pamoja na tisho la wanamgambo wa Al Shabaab ambao wametishia
kuipindua wakisema inaungwa mkono na nchi za Magharibi.


No comments:
Post a Comment