Viongozi wapya wa TASJA wakiwa katika
picha ya pamoja waliokaa kulia ni Mwenyekiti mpya Greyson Mutembei na
Katibu Mkuu wake Benard Lugongo wakiwa na baadhi ya wajumbe wapya wa
kamati ya utendaji.
CHAMA cha Waandishi wa habari za
Sayansi nchini (TASJA), kimepata viongozi wapya watakiongoza chama hicho
kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Waliochaguliwa ni Pamoja na Greyson
Mutembei, ambaye ni Mwenyekiti mpya, Bakari Kimwanga Makamu Mwenyekiti,
Benard Lugongo Katibu Mkuu na Nasra Abdallah Mweka hazina.
Mbali mkutano huo umewachagua wajumbe
wa kamati ya uttendaji ambao ni David Ramadhan, Asia Rweymamu, Gabriel
Mushi, Restusta James, Jackob Nduye na Hamis Shimye.
Awali akifungua mkutano Mkuu huo
wa mwaka, mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda, alisema ili nchi iweze
kuendelea inahitaji wanasansi na wabuni wengi ambao wataleta maendeleo
nchini.
“Tunajua TASJA kwa namna mlivyo
mnaweza mkawa chachu ya maendeleo katika sekta ya Sayansi nchini, nasi
kama wadau wakuu tunaamini waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika
wakuelimisha wananchi.
“Ahadi yangu kwenu TASJA kupitia
COSTECH mnafika mbali sambamba na kuwaunganisha na taasisi zingine
kimataifa,” alisema Dk. Mshinda Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara
na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama, alisema
kuwa hivi Maendeleo ya teknolojia za mawasiliano yamejkuwa yakichukua
nafasi kubwa katika maendeleo ya Taifa.
“Kwetu TPC tumejiandaa katika kutoa
huduma zatu ikiwemo EMS, Post Cargo na Inateranet ambayo imekuwa
ikitumiwa na watanzania wetu nanyi TASJA ni moja ya wadau wetu,”alisema
No comments:
Post a Comment