Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas
Massaburi (kushoto) akikabidhiwa gazeti jipya la Dar Metro na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited
inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee,
Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara
mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji. (PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA)
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas
Massaburi (kushoto) akisoma gazeti jipya la Dar Metro alilopelekewa na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited
inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee,
Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara
mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji.Kampuni hiyo huchapisha pia
magazeti ya Jambo Leo, jarida la Jambo Brand Tanzania na Staa Spoti.
(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Massaburi akilipitia vizuri gazeti hilo litakalokuwa linaandikwa kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Pinto akizungumza na Massaburi
No comments:
Post a Comment